Kama utakuwa mtazamaji mzuri wa vipindi vya TV Tanzania
basi utakuwa ushazoea kuona tamthilia za kiphilipino ambazo huwa
zinaoneshwa katika vipindi vya TV stations mbalimbali Tanzania. April 19
2016 mashabiki na wapenzi wa tamthiliya Tanzania wamepewa good news.
Msanii wa filamu Tanzania Suzan Lewis ‘Natasha’ na msanii filamu na muhadhiri wa Chuo kikuu Issa Mbura ambaye alijipatia umaarufu katika filamu ya Coming Home wameingia katika mpango wa Azam TV kuandaa na tamthilia ya Taxi itakayoanza kuruka mwezi June.
Washiriki wa tamthilia hiyo ya Taxi
watapatikana baada ya kufanyiwa usahili kesho April 20 2016 katika
ufukwe wa Coco beach lakini pia watapatiwa mafunzo ya kuigiza ya
kimataifa ili tamthilia ya Taxi iweze kuwa nzuri kama zilivyo baadhi ya tamthilia.

Maoni
Chapisha Maoni