Nauli Daraja la Kigamboni Kuanza Kutozwa Mei Mosi
| Eng Karim Mataka |
Meneja Mradi kutoka NSSF, Mhandisi Karim
Mataka amesema baadhi ya Madereva wamekuwa wakikiuka taratibu/sheria na
alama zilizowekwa katika daraja la Kigamboni ambalo ni kubwa Afrika
Mashariki ambalo linatarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 100 iwapo
litapata matunzo stahiki.
Daraja hilo ambalo litaanza kutumika rasmi kwa kulipia Mei Mosi 2016, Mhandisi Karimu amewataka Watanzania kulinda miundo mbinu ya daraja hilo ikiwemo kutii sheria zote za Daraja hilo ili kuepuka kusababisha uharibifu wa aina yoyote ile,kwa sababu limejengwa kwa gharama kubwa na linahitaji matunzo.
Mhandisi alibainisha pia kuwa Daraja hilo la Kigamboni ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na kulibatiza jina la Daraja la Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Maoni
Chapisha Maoni