Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Obama na Merkel - Ukumbatiaji wa kimkakati

Maoni: Obama na Merkel - Ukumbatiaji wa kimkakati

Rais wa Marekani, Barack Obama, alidhihirisha jinsi alivyo karibu na kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Hii ilidhihirisha hisia za kibinadamu alizonazo na fikra zake kimkakati,
Deutschland Angela Merkel Barack Obama Hannover Messe Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Marekani Barack Obama, Hannover
Ingawa Obama amejitolea kumfunza Merkel kucheza mchezo wa gofu, rais huyo wa Marekani anayejiandaa kuondoka madarakani anategemea kwamba kansela Merkel hatalikubali pendekezo hilo wakati wowote hivi karibuni.

Sababu iko wazi: miezi michache kabla kuondoka madarakani, Obama anaona mambo aliyoyafanikisha kisiasa na urithi wake kisiasa viko hatarini. Mwenendo wa dunia, ulioundwa na muungano kati ya Marekani na Ulaya baada ya kumalizika vita vikuu vya pili vya dunia, unaonekana kuyumba zaidi kuliko ilivyoshuhudiwa awali baada ya mihula yake miwili ya urais.

Vita vipya baridi vinaibua wasiwasi kuhusu amani ya Ulaya na imeifanya Ukraine kuwa eneo ambalo Urusi inamenyana na mataifa ya magharibi kung'ang'ania madaraka. Wanamgambo wa kigaidi wa Mashariki ya Kati wanaonekana kulisukuma eneo hilo katika ukingo wa kujiangamiza lenyewe. Na katika kipindi ha miezi kadhaa, mzozo wa wakimbizi ulitoa changamoto kubwa kwa historia ya miongo kadhaa ya mfungamano wa Ulaya.

Obama anaandaa mazingira ya kukabidhi madaraka
Bila shaka Obama kumkaribia Merkel ni mkakati: Rais huyo wa Marekani atakapokabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani, atamhitaji mtu atakayeyaendeleza maono namisimamo yake ya siasa za ulimwengu. Nchini Marekani watu wengi wana wasiwasi kama mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump anaweza kutegemea iwapo atashinda katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Fuchs Richard Kommentarbild App Mwandishi wa DW, Richard Fuchs

Mtizamo kwamba mvutano kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu mzozo wa wakimbizi unaweza kumfagia na kumyumbisha kisiasa kansela Merkel anayeonekana kuwa nembo ya uthabiti, kunaweza kuwa jinamizi la siasa za dunia kwa Obama. Hii ndio sababu kwa nini Obama anatumia nguvu zake zote zilizobakia za kisiasa katika kuimarisha mahusiano yanayoendelea katika ngazi zote zinazostahiki kwa kutumia nyenzo zifaazo. Na kwa sababu hiyo, anakubali kwa makusudi makabiliano na wapinzani kadhaa wa sera za uhamiaji za kansela Merkel.

Uumoja wa Ulaya ukivurugika, hakutakuwa na ulimwengu huru
Miradi ya pamoja inatakiwa isaidie kuandaa mazingira ya mambo mapya, kama mijadala kuhusu mzozo wa wakimbizi ambao unalileta pamja bara la Ulaya. Kwa Obama mkataba wa kibiashara kati ya Marekani na Ulaya ni kitu kiachounganisha ambao anataka kuutumia kuleta msukumo mpya kwa mjadala kuhusu uhusiano kati ya Marekani na mataifa ya Ulaya - na yeye anataka kumuweka kansela

 Merkel awe mratibu wa mkataba huo mpya wa kibiashara kati ya pande hizo mbili. Merkel kama mdhamini wa umoja katika bara la Ulaya ana jukumu la ziada katika suala hilo. Obama anachukulia kwamba Merkel atahakikisha umoja barani Ulaya.

Rais Obama anahisi kumetokea ombwe la kisiasa barani Ulaya. Imani ya mradi wa pamoja wa kuwa na Ulaya yenye umoja imemomonyoka. Umoja huu ni wa umuhimu, sio tu kwa Ulaya, bali pia kwa maeneo mengine ya ulimwengu ulio huru, anaamini Obama.

Wasiwasi wake kuhusu taasisi kama bvile Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, ni wa msingi. Bila kuwa na muungano imara kati ya Ulaya na Marekani taasisi hizi zilizoundwa baada ya kumalizika vita vikuu vya pili vya dunia, hazitaendelea kuwepo kwa muda mrefu katika siasa za dunia karne ya 21.

Kwa sababu kwa kansela Merkel ulimwengu ulio huru ni muhimu sana, binafsi amekuwa mtu ambaye rais Obama analazimika kushirikiana naye kwa karibu na hawezi kumuacha. Pia ni sehemu ya mkakati wake rais Obama kumkumbatia kansela huyo wa Ujerumani. Kwa hivyo msaada kwa Merkel utakuwa sehemu muhimu ya urithi wa kisiasa wa Obama.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.