![]() |
| Suarez |
Atletico na Real Madrid zimezidi kuiongezea presha
Barcelona, lakini mabingwa hao wa La Liga wamezidi kukaza buti mbio za
ubingwa msimu huu Suarez akitenda miujiza
Kutoka kwenye majanga ya vipigo, Barcelona imekuja na moto mkali kwa ushindi mkubwa kwenye mechi mbili mfululizo wakianza na ule wa bao 8-0 dhidi ya Diportivo kabla ya ushindi wa Jumamosi usiku.
Messi alianza kuzifungua kamba za Sporting Gijon mapema kipindi cha kwanza akifunga bao moja pekee kati ya mabao sita yaliyofungwa kwenye mchezo huo.
Baadaye Luis Suarez alipachika bao la pili na matokeo kuwa 2-0. Penalti mbili za haraka-haraka zilizofungwa na Suarez ziliyafanya matokeo kuwa 4-0.
Dakika tano kabla ya mchezo kumalizika ikapatikana penalti nyingine ambayo iliwekwa kimiani na Neymar hivyo kuifanya safu ya ushambuliaji ya Barca (MSN) kila mmoja kufunga bao kwenye mchezo huo
Suarez akapiga bao lake la nne kwenye mchezo huo dakika za lala salama na kukamilisha ushindi wa Barcelona 6-0 Sporting Gijon.
Kwa mwendo huo hadi sasa, Luis Suarez amefikisha mabao 34 Cristiano Ronaldo akiendelea kubaki na mabao yake 31 baada ya kukosa mechi ya Rayo Vallecano. Mbio za tuzo ya Pichichi!
Zikiwa zimesalia mechi tatu,
Barcelona inaongoza ligi kwa pointi 82 sawa na Atletico Madrid huku Real
Madrid ikifuatia kwa pointi zake 81.

Maoni
Chapisha Maoni