Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea
tena leo April 27 2016 kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja vya
Chamazi na Taifa, uwanja wa Chamzi Azam FC walicheza dhidi ya Majimaji
FC ya Songea, wakati uwanja wa Taifa Yanga waliwakaribisha Mgambo JKT ya
Tanga.

Kwa upande wa Yanga bado wao wanaonesha
hawataki mchezo wa kutegemea matokeo ya mechi nyingine, kitu ambacho
kimewafanya wawe na juhudi ya kushinda kila mchezo, kwani Azam FC na
Simba nafasi zao za kuwania au kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania bara
msimu huu inategemea Yanga kama watapoteza au kupata sare katika mechi
zake.
Katika mchezo uliochezwa Taifa Dar es
Salaam Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Mgambo
JKT, Nassoro Gumbo ndio alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli dakika
ya 4 na kuifanya Mgambo kuongoza kalba ya Deus Kaseke kuifungia Yanga
magoli mawili muhimu dakika ya 44 na 72.
Maoni
Chapisha Maoni