Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wenger ahofia Arsenal kushindwa kufuzu Uefa


Gunners wameishiwa mbinu na Kocha wao Mfaransa amezidi kuchanganyikiwa huku akiwa na hofu ya kushindwa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Uefa

Arsene Wenger amekiri kwamba anahofu Arsenal haina uhakika wa kutinga nne-bora baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Sunderland.

Arsenal walishindwa kuwafunga Paka Weusi, ambao pointi moja katika uwanja wao wa nyumbani imewapa tumaini la kupona kushuka daraja.

Petr Chech alilazimika kuokoa shuti kali kutoka kwa Wahbi Khazri na Jermain Defoe, Arsenal wakishindwa kuonyesha umahiri wa kikosi chao kutumia nafasi walizopata.

Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kubakia nafasi ya nne, pointi tano mbele ya Manchester United – ambao wana mchezo mmoja mkononi hali inayomfanya Wenger kuwa na hofu katika mechi zilizo mbele yao, moja ikiwa ni dhidi ya Manchester City na nyingine dhidi ya Norwich inayohaha kujiokoa kushuka daraja.

Alipoulizwa kama anahofu Arsenal itapoteza fursa ya kupata nafasi ya 4-bora, Wenger alisema: “Naam, ndiyo. Tunaogopa kwa sababu haya ni mapambano.


“Kuna ligi mbili kwa sasa: timu tunazodhani ni rahisi – unakuta zinacheza vizuri, zikiwa zinapambana kuepuka kushuka daraja, na mchezo unakuwa tofauti.

 “Inaumiza kwa sababu tunacheza ili kushinda taji na hali halisi kwamba hatushindi ni moja ya mambo yanayoleta kero, sawa natimu nyingine nyingi
.
“Timu kama Sunderland wapo tayari kupambana kufa na kupona, na hawakati tamaa dakika zote 90.
“Walianza kwa hofu na tungeweza kutumia udhaifu huo walioanza nao, lakini hatukuweza ukizingatia tulicheza Jumapili, Alhamisi, na leo [Jumapili], tulikuwa na uchovu kiasi fulani na matokeo yakawa hivyo.”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.