Ruka hadi kwenye maudhui makuu

C. Ronaldo – Rekodi 2 anazoweza kuzivunja, ataweza kuondoa ukame wa San Siro, na vitu wanavyotakiwa kufanya Atletico kumzuia asiwadhuru

C. Ronaldo – Rekodi 2 anazoweza kuzivunja, ataweza kuondoa ukame wa San Siro, na vitu wanavyotakiwa kufanya Atletico kumzuia asiwadhuru

Cristiano Ronaldo alifunga mara ya mwisho Real Madrid walipokutana na Atletico katika fainali ya UEFA Champions League, lakini je atafanikiwa kuwafunga tena? Tuangalie takwimu muhimu kuhusu Cristiabo Ronaldo kuelekea mchezo huu.
image
1. Rekodi za kuvunja
Ikiwa kuna rekodi za kuvunja basi Cristiabo Ronaldo atajaribu kuzivunja; kwenye fainali ya Jumamosi kuna kuna rekodi kubwa tatu za kuvunja. CR7 ameshafunga magoli 16 katika mashindano haya msimu huu na anahitaji goli lingine ili kuifikia rekodi yake ya kufunga magoli mengi zaidi katika msimu mmoja wa UCL – rekodi aliyoiweka msimu wa 2013/14. Pia anaweza kuifikia rekofi ya Lionel Messi kuwa mfungaji bora katika misimu minne mfululizo.
image
Anaweza pia kumzidi Messi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali 3 za Champions League. Ronaldo ni mmoja ya wachezaji 16 ambao wameshafunga katika fainali mbili za ulaya, lakini pia ana safari ndefu ya kuifikia rekodi ya Alfredo di Stefano ya kufunga magoli katika mechi 5 za fainali za ulaya (1956, 1957, 1958, 1959, 1960)
image
Kufunga goli ndani ya San Siro – Milan
Stadio San Siro ni uwanja mgumu kwa Ronaldo, hajawahi kufunga goli katika uwanja huo. Ameshacheza dakika 360 za  UEFA Champions League kwenye uwanja huu – mechi 3 na Manchester United na moja na Real Madrid – lakini hajawahi kufunga goli – au kuwa katika kikosi kilichoshinda katika uwanja huu.

Rekodi za Cristiano Ronaldo katika uwanja wa San Siro  (W0 D2 L2)
AC Milan 2-2 Real Madrid, 03/11/10
Internazionale 0-0 United, 24/02/09
AC Milan 3-0 United, 02/05/07
AC Milan 1-0 United, 08/03/05
Kufunga vs Atletico
Nahodha huyo wa Ureno ameshaifunga Atletico Madrid magoli 15 katika mechi 24 – katika michuano ya La Liga, Copa, Spanish Super Cup – hat trick moja katika ushindi wa 4-1 ugenini mnamo April 2012, ameshawahi kupewa kadi nyekundu katika fainali waliyofungwa 2-1 ya Copa del Rey.
image
Kwa ujumla amecheza dakika  2,117 dhidi ya Atletico, ana wastani wa kuwafunga katika kila dakika 141. Japokuwa kwa sasa ana ukame wa kutokuwafunga katika 487 – mara ya mwisho kuwafunga ilikuwa kwenye mchezo wa Copa del Rey waliotoka sare ya 2-2 mnamo January 2015.
image
Vitu wanavyotakiwa kufanya Atlético ili asiwadhuru.
1) Kujihadhari na penati; magoli 7 kati ya 15 aliyowafunga Ronaldo yalitokana na mikwaju ya penati.
2) Kumpa udhibiti maalum katika dakika 25 za mwanzo za mchezo; takwimu zinaonyesha katika magoli 15 aliyowafunga – 8 aliyafunga ndani ya dakika 25 za mwanzo na manne kati ya hayo ni katika dakika ya 22 mpaka ya 25.

Takwimunza Cdistiano Ronaldo vs Atletico katika mechi zote.(W12 D5 L7)
90: Madrid 3-2 Atlético, 28/03/10
90: Madrid 2-0 Atlético, 07/11/10
90: Madrid 3-1 Atlético, 13/01/11 (Copa del Rey) – one goal: 60
90: Atlético 0-1 Madrid, 20/01/11 (Copa del Rey) – one goal: 22
70: Atlético 1-2 Madrid, 19/03/11
90: Madrid 4-1 Atlético, 26/11/11 – two goals: 23pen, 82pen
90: Atlético 1-4 Madrid, 11/04/12 – three goals: 24, 67, 82pen
90: Madrid 2-0 Atlético, 01/12/12 – one goal: 15
115: Madrid 1-2 Atlético, 17/05/12 (Copa del Rey) – one goal: 14, shown red card in extra-time
90: Madrid 0-1 Atlético, 28/09/13
90: Madrid 3-0 Atlético, 05/02/14 (Copa del Rey)
74: Atlético 0-2 Madrid, 11/02/14 (Copa del Rey) – two goals: 6pen, 15pen
90: Atlético 2-2 Madrid, 02/03.14 – one goal: 81
120: Madrid 4-1 Atlético, 24/05/14 (UEFA Champions League final) – one goal: 120pen
44: Madrid 1-1 Atlético, 19/08/14 (Spanish Super Cup)
45: Atlético 1-0 Madrid, 22/08/14 (Spanish Super Cup)
90: Madrid 1-2 Atlético, 13/09/14 – one goal: 25pen
28: Atlético 2-0 Madrid, 07/01/15 (Copa del Rey)
90: Madrid 2-2 Atlético, 15/01/15 (Copa del Rey) – one goal: 53
90: Atlético 4-0 Madrid, 07/02/15
90: Atlético 0-0 Madrid, 14/04/15 (UEFA Champions League quarter-final)
90: Madrid 1-0 Atlético, 22/04/15 (UEFA Champions League quarter-final)
90: Atlético 1-1 Madrid, 04/10/15
90: Madrid 0-1 Atlético, 27/02/16

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.