Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Dalili hizi zinaonyesha kuwa unaelekea kuwa maskini

Dalili hizi zinaonyesha kuwa unaelekea kuwa maskini


Baada ya shule, kama vijana tunafanya jitihada za kutafuta kazi tuwe na maisha mazuri, kwa maneno mengine naweza kusema, tuondokane na umaskini.

Katika kupigania hilo tunajikuta tunaendesha maisha fulani ambayo yanatulevya na baadaye tunajikuta hatuna tena nguvu ya kuyabadilisha. Tunaingia katika madeni ili tuweze kuyaendesha maisha hayo ya mapicha picha. Alafu mioyoni tunajidanganya kwamba  hayo ni maisha mazuri na yanaonyesha sie tuna uwezo.

Unaweza kuishi maisha ya sinema, kwamba kila mtu akuone una hiki na kile wakati kiukweli ukiangalia wewe ni maskini wa kutupwa. Unaweza kuwa na kazi yenye mshahara mkubwa  na huo mwenendo wa maisha yako ukakudanganya kwamba unaelekea pazuri lakini kiukweli ikawa ni kinyume kabisa.

Utajuaje kama sasa huku ninakoelekea nitakua maskini? Angalia hizi dalili na kama utakua uko katika kipindi cha mwanzo cha kuajiriwa ikusaidie ili usijikute kwenye mashimo yaliyowachota wengi.

Kwanza, huwezi kuishi bila Mshahara wako, kiasi mshahara ukicheleweshwa wiki moja tu unaandamana mitaani, au mishahara ya miezi miwili haikutani. Wote wanaanza kama hivi, tunahitaji mishahara  kulipa kodi, kununua chakula, kulipa ada za watoto, na nyingine tuweze ku-enjoy kidogo, hakuna anayebisha katika hili, lakini unashauriwa hili lisiwe la muda mrefu, unapoanza kazi jitahidi ifikie muda uweze kuishi bila kutegemea mshahara wako. Isiwe mshahara ukicheleweshwa basi wewe ni kulia njaa tu.

Kulifanikisha hilo inamaana kipande cha mshahara wako inabidi ukihifadhi, na kadri unavyokua ndo kipande hicho unachokata kwa ajili ya kuhifadhi kiongezeke na chenyewe. Na vile vile uweze kuwekeza. Story za wewe kuhamia kwenye jumba kubwa, kwenda baa za bei ghali, magari makubwa waachie Bongo movies, wao ndo wana haki ya kuigiza hata maisha yao maana kazi yao kubwa ni uigizaji. Hayo yote kwako yanakufanya tu uendelee kutegemea mshahara wako.

Sababu nyingine ni kumiliki vitu vingi vyenye thamani ya pesa lakini visivyodumu. Kuwa na gari zaidi ya moja tena ya bei mbaya, TV imeziba ukuta mzima na mengineyo, na gharama ya hivyo vyote vinazidi kile ulichokiwekeza kwenye hisa, Biashara au vitu vingine vyenye thamani isiyopungua kama Ardhi.

Ikiwa hivi rafiki yangu nakushauri ufanye kinyume, ikiwezekana uza kabisa hiyo TV ukanunue Hisa TBL au TCC. Gari ulilonunua leo milioni 30, mwakani huwezi kuliuza kwa milioni 30, na hata kama utauza milioni 30, uwezo wa milioni 30 hiyo hautakua ni ule wa mwaka jana. Fanya uamuzi kwa makini, wekeza pesa zako sehemu au kwenye vitu visivyopungua thamani. Na kwamwe usije uza vitu kama ardhi ili ununue gari, au uende likizo.

Ukijikuta unatumbua fedha zako kumfurahisha fulani. Tunalazimika kuamini kwamba, simu tunazotumia, sehemu tunazoishi, magari tunayoendesha au viwanja tunavyoenda kufurahi vinatujengea heshima fulani katika jamii, niamini mimi ‘no body cares’ ukifeli maishani unakua ni wewe na Mungu wako. Hao unaodhani wanauheshimu kwa unachokifanya hawatakuwepo na si ajabu wakaanza kukukimbia mtaani ukitokeza tu.

Alafu ni adhabu, maana kama watu walikuheshimu kisa ulikuwa na Passo cc 1000 sasa inabidi usishuke chini, upande juu kwenye Brevis cc 2000, kumbuka na matumizi ya mafuta yanapanda, unazidi kupunguza kipande chako cha kuwekeza. Huu mzunguko unaendelea mpaka inafika kipindi unaishiwa kabisa. Kutumia fedha ulizozipata kwa jasho lako haijawahi kuwa mbaya, tena tunaamini utakapotumia ndo nguvu ya kutafuta nyingine inakuja haraka, ubaya ni pale unapokua na maamuzi mabaya juu ya matumizi yako.

Na vile vile unapochukua mkopo ili utumie na wala sio kufanya ule mkopo uzalishe kitu fulani. Hii inamaanisha ulichukua mkopo uendeleze yale maisha yako ya picha picha na wala haukuzalisha chochote. Mwisho wa siku, mikopo ya aina hii inakufanya uanze kutumia zaidi ya kipato chako. Hatusemi usikope kabisa, kopa kwa misingi ya kuzalisha kitu, hata mkopo ukirudi unakua na kiasi Fulani cha fedha ambacho aidha utakitumia au kukiwekeza kwa manufaa yako.

La mwisho ninaloweza kuongelea leo ni kuwa na mipango katika maisha yako.  Kama utapangilia vizuri maisha yako, umasikini utaishia kuuona kwene TV na kusikia tu kutoka UN kwamba kuna Watanzania wanaoishi chini ya dola 1. Njia unayochukua au kuchagua maishani mwako hakikisha inakupeleka sehemu ambayo ukikaa chini wewe mwenyewe uangalie nilikua huku na sasa niko hapa.

 Na hakuna mwingine atakaekuja kukuwekea msimamo wa wewe kujitegemea zaidi yako. Na siku zote kwa kuangalia ni mwanzo wala sio mwisho. Ukianza na misingi mizuri utafika pazuri.

Unatakiwa ifike mahali useme kazi au biashara yangu niliyofanya kuanzia mwaka Fulani mpaka mwka Fulani, imenisaidia kufanya hiki na kile. Na ukiwa na mipango yako unayotakiwa kukamilisha, ni lazima utajipimia hata katika matumizi yako ili uweze kufikia malengo yako. Miasha ya mapicha picha tuyaache huko huko Instagram kwa waigizaji.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.