Mfano magari madogo yanayotumika sana na watu binafsi yatatakiwa kulipia shilingi 1500 kila yanapopita juu ya daraja hili lakini kwenye taarifa ya kwanza haikufafanua kama mtu analipia kwa siku ama kwa kila anapopita na ndio maana baadhi ya Wakazi wa Kigamboni walitaka kujua kama kwa wao kuna punguzo lolote hasa wanaopita zaidi ya mara moja kwa siku.
Injinia Karim Mattaka ambaye ni Meneja kwenye mradi wa daraja hili ameongea na kusema bei zilizotajwa ni za kupita mara moja hakuna utaratibu mwingine zaidi ya hapo, utalipia kwa kadri unavyopita hata kama ni mara sita kwa siku utalipia safari zote sita.
Kwa alichokisema Injinia hapo juu ni wazi kabisa hakutokua na punguzo maalum au huruma kwa baadhi ya Wakazi wa Kigamboni ambao walipaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kufikiriwa kwakuwa watapita mara nyingi kwa siku juu ya daraja hilo

Maoni
Chapisha Maoni