Donald Trump njia nyeupe Urais Marekani
Mtia
nia wa Chama cha Republican cha Marekani Donald Trump amefikisha idadi
ya wajumbe wanaohitajika kufikiwa na chama ili kuweza kuteuliwa kugombea
Urais.
Donald Trump aliwashinda wapinzani
wenzake 16 ndani ya chama cha Republican. Imearifiwa kuwa Donald Trump
amefikisha wajumbe 1,238, mmoja zaidi ya waliokuwa wanahitajika.
Kufuatia hatua hiyo kubwa kwa Donald
Trump, ni dhahiri kuwa sasa njia itakuwa nyeupe kwake kuweza kuteuliwa
kupeperusha bendera ya Republican katika uchaguzi mkuu wa Marekani
utakaofanyika Novemba mwaka huu.
Maoni
Chapisha Maoni