Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Faida ya Safaricom yafika $381m

Faida ya Safaricom yafika $381m

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom nchini Kenya imetangaza ongezeko la asilimia 19.6 katika faida yake ya mwaka wa kifedha uliomalizika Machi mwaka huu baada ya kutozwa kodi, ikisaidiwa sana na ukuaji wa mapato kutoka kwa M-Pesa na data.

Kampuni hiyo ilipata faida ya Sh38.1 bilioni ($381 milioni) baada ya kutozwa kodi kutoka Sh31.87 bilioni ($318.7 milioni) ilizopata mwaka wa kifedha uliotangulia.

Mapato kutoka kwa M-Pesa yaliongezeka asilimia 27.2 na kufikia Sh41.5 bilioni ($415 milioni) katika kipindi hicho huku idadi ya wateja wanaotumia huduma hiyo na kutuma na kupokea pesa angalau siku moja kwa mwezi ikipanda asilimia 17.5 hadi 16.6 milioni.

Jumla ya thamani ya shughuli za kibiashara zilizofanywa kupitia M-Pesa ilipanda asilimia 27 hadi Sh5.29 trilioni ($52.9 bilioni).

Mapato kutoka kwa data yalikua asilimia 42.7 na kufikia Sh21.2 bilioni ($212 milioni), wateja wanaotumia data kupitia simu zao angalau mara moja kwa mwezi wakiongezeka asilimia 21.5 hadi 14.1 milioni.

Kufikia Desemba mwaka 2015, Safaricom ilikuwa ikiongoza kwa kuwa na wateja wengi nchini Kenya, ikiwa na asilimia 64.7 ya wateja wote. Idadi hiyo hata hivyo ilikuwa imeshuka kutoka asilimia 67 jambo ambalo kampuni hiyo inasema lilitokana na kubadilishwa kwa mfumo wa kuhesabu wateja.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.