Granit Xhaka rasmi Arsenal
Klabu ya Arsenal imemsajili kiungo
wa kati wa timu ya taifa ya Switzerland Granit Xhaka kutoka klabu ya
Borussia Monchengladbach.
''Nafurahia kujiunga na Arsenal'',alisema Xhaka.''Nataka kuhamia mjini London ili kuiwakilisha kilabu hii na kucheza katika ligi ya Uingereza''.
''Nitafanya kila kitu kuwapatia taji Arsenal na kuwafurahisha mashabiki''.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alisema: Granit Xhaka ni mchezaji mzuri aliye na uzoefu wa michuano ya vilabu bingwa Ulaya na ile ya Bundesliga.
''Tumekuwa tukimfuatilia kwa mda mrefu na ni mchezaji atakayeongeza maarifa katika kikosi chetu''.

Maoni
Chapisha Maoni