Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Habre afungwa maisha jela

Habre afungwa maisha jela

Aliyekuwa dikteta wa Chad, Hissene Habre, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya maelfu ya watu wakati wa utawala wake.
Aliekuwa dikteta wa Chad Hissene Habre Aliekuwa dikteta wa Chad Hissene Habre
Dikteta huyo wa zamani alipewa adhabu hiyo kwenye mahakama maalumu ya mabaraza ya Afrika, katika mji mkuu wa Senegal, Dakar. Jaji Gberdao Gustave Kam alisema wakati wa kuitoa hukumu hiyo.
"Kutokana na hayo Hissene Habre, mahakama inakuhukumu kifungo cha maisha jela."

Nderemo baada ya hukumu kutolewa
Mamia ya watu walishangilia baada ya Habre kupewa adhabu hiyo mjini Dakar. Waliokuwa wafungwa wakati wa utawala wake walikumbatiana kwa furaha kubwa huku wenye magari wakipiga honi!

Habre alipatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya maalfu ya watu wakati wa utawala wake kuanzia mwaka wa 1982 hadi 1990.

Tume ya ukweli iliyoundwa mnamo mwaka wa 1992 nchini Chad imemlaumu dikteta huyo wa zamani kwa kuweka mfumo wa mateso na imesema kwamba watu 40,000 waliuawa wakati wa utawala wake. Tume hiyo imelinyooshea kidole hasa jeshi la polisi.
Mkutano na waandishi habari mjini Dakar juu ya Habre Mkutano na waandishi habari mjini Dakar juu ya Habre
Habre ameishutumu hukumu iliyotolewa dhidi yake na amesema imetokana na sababu za kisiasa. Habre na wafuasi wake, mara kadhaa walijaribu kufanya fujo mahakamani kwa kupiga kelele na kuimba.Hapo awali alikataa kutetewa na mawakili lakini mahakama iliwateua wanasheria wa Senegal ili wamtetee.Habre amekuwa anaishi nchini humo tangu akimbie Chad mnamo mwaka wa 1990.

Deby aunga mkono hukumu
Rais wa Chad Idris Deby aliekuwa mshauri wa masuala ya kijeshi wa dikteta Habre,kabla ya kumtimua madarakani ,ameunga mkono adhabu iliyotolewa na mahakama.
Kesi ya Habre imefanyika kutokana na juhudi za watu waliofungwa jela wakati wa utawala wake. Watu hao wamekuwa wanaendesha kampeni ya kumfikisha mahakamani.

Wakili wa asasi ya haki za binadamu ya Human Rights Watch, Reed Brody ameeleza kwamba Habre alifikishwa mahakamani siyo kutokana na juhudi za waendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa,ICC ya mjini the Hague na wala siyo kutokana juhudi za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, bali ni kutokana na juhudi za watu wa Chad wenyewe waliokumbwa na uhalifu uliotendwa na dikteta huyo wa zamani.

Kesi hiyo iliyosikilizwa na mabaraza maalumu ya Afrika na kufanyika nchini Senegal ilianza mnamo mwezi Julai mwaka uliopita.

Hii ni mara ya kwanza kwa mtawala wa zamani kuhukumiwa na mahakama za nchi nyingine kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu. Mahakama maalumu iliyosikiliza kesi ya Habre iliundwa na Senegal kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika. Kesi nyingine juu ya fidia kwa kwa asasi za kiraia zaidi ya 4000 itafanyika katika siku zijazo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.