Jaji kaamua hivi kuhusu ile Kesi ya Ciara na Future kuhusu mtoto.
Drama kati ya rnb staa Ciara na Future zinaendelea na wiki hii kesi yao kuhusu mzazi yupi ana haki ya kuwa na muda zaidi wa malezi ya mtoto wao ‘Future’ imechukua hatua nyingine.
Jumatatu hii jaji mjini Los Angeles ameruhusu Future awe na haki sawa za kuwa na mtoto wao Future na kwamba Ciara atagawanya muda wake na mtoto wao pamoja na Future.
Ciara alifungua kesi hio akidai baba wa mtoto wake sio mtu mzuri kabisa, Ciara kwa sasa ni mwanamitindo wa kampuni ya IMG Models na atasherehesha tuzo za Billboard Music Awards pamoja na rapa Ludacris.
Maoni
Chapisha Maoni