Kipre Tchetche ajasaini Oman
Baada ya kuenea kwa habari za
mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Azam FC
Kipre Tchetche kuripotiwa kusaini klabu ya Nahda Al-Buraimi ya Oman,
afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba ameeleza ukweli na
kuwatoa hofu mashabiki walioshtushwa na habari hizo.
C.E.O wa Azam FC Saad Kawemba kaeleza
kuwa hizo ni habari za uzushi za kuwa nyota wao amesaini Nahda
Al-Buraimi ya Oman, kwani bado ana mkataba na Azam FC ndio maana hata
vyombo vya habari vinaripoti kuwa anaomba akapate changamoto mpya kwa
maana ana mkataba na Azam FC.
“Kipre
ni mchezaji wetu ambae ni muhimu huwezi kumruhusu amalize msimu aende
mapumziko akiwa hana mkataba, kwa hiyo tuna mkataba ambao ni endelevu,
nadhani ndio maana ukasikia wanasema anaomba akapate changamoto sehemu
nyingine, ukweli ni kuwa mchezaji kama ana mkataba ni makubaliano umuuze
au anunue mkataba”

Maoni
Chapisha Maoni