Mamia mkoani Mbeya wajitokeza kumzika Kinyambe
Mamia ya watu wamejitokeza Ijumaa hii mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi ya mchekeshaji maarufu nchini Tanzania kutoka katika Kundi la Vituko Show, Mohammed Abdallah ‘Kinyambe’ aliyefariki dunia Jumatano iliyopita akiwa katika hospitali ya Mbeya.
Mmoja kati ya wasanii wanaounda Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania, Mkono Mkonole, kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika:
Kila nafsi itaonja umahuti kwa heri kinyambe kila mwanadamu huu ndio mwisho wake pumzika kwa amaniMkonole Alhamisi hii alisema kuwa Kinyambe alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni mpaka anapatwa na umahuti akiwa nyumbani kwao Mbeya.
Mazishi yake yamehudhuriwa na wananchi, wadau wa filamu pamoja na wasanii wenzake wa filamu ambao walisafikiri kutoka Dar es salaam.
Maoni
Chapisha Maoni