Mayweather athibitisha kuzichapa na Conor McGregor
Mayweather amethibitisha kuwa atazichapa na staa wa UFC, Conor McGregor kwa kupost picha hiyo juu kwenye Instagram. Post hiyo hata hivyo haioneshi ni lini pambano hilo litafanyika ingawa limepigia mstari ujio wa pambano hilo linalodaiwa kuja kuwa la thamani zaidi kwenye historia ya ndondi duniani.
Conor McGregor naye ametumia picha kupost picha hiyo chini. “MMA Vs Boxing,” aliandika kwenye picha hiyo.
Hata hivyo inadhaniwa kuwa pambano hilo litapigwa September mwaka huu.
Maoni
Chapisha Maoni