Mfahamu mmiliki mpya wa Aston Villa Tony Xia toka China
Japokuwa Dr Tony Xia ni miongoni mwa watu wenye fedha duniani, lakini si mtu anayefahamika sana. Historia yake katika mpira, chanzo cha fedha zake na vingine vingi ni wachache sana wanavifahamu.
Hapa tunakuwezesha wewe kufahamu mmiliki mpya wa klabu ya Asto Villa.
Dr Tony Xia ni nani?
Tony Xia alizaliwa katika Mji wa Quzhou ambao uko umbali wa maili 250 kusini magharibi mwa Shanghai. Baba yake alikuwa ni mkulima na mama yake alikuwa ni mama wa nyumbani. Kutokana na uwezo wake mzuri aliouonyesha darasani, alienda Marekani kusoma katika Chuo Kikuu cha Havard na MIT na wakati huo huo akichukua kozi ya miezi 5 katika Chuo cha Oxford.Ametoa wapi uwezo wa kununua Aston Villa?
Bado haijafahamika kiasi halisi cha utajiri anachomiliki lakini huwezi kuacha kumuweka katika kundi la mabilionea. Anamiliki moja ya kampuni kubwa ambayo imeajiri takribani watu 35,000 katika nchi 75. Recon Group ni moja ya makampuni ya kimataifa, ni kampuni hii hujishughulisha na mambo mengi ikiwa ni pamoja na Information Technology (IT), Afya, Uhandisi, Usafrishaji na Michezo.Ameinunua klabu ya hiyo kwa kiasi cha Euro milioni 60, lakini fedha hizo zitapanda na kufika Euro milioni 100 kama klabu hiyo itafanikiwa kupanda daraja. Huu ni moja kati ya uwekezaji mkubwa kufanyika katika ukanda wa China.
Je! anauzoefu gani katika masuala ya mpira?
Xia alikuwa akisakata kabumbu hadi alipomaliza chuo na pia amekuwa akitamani sana kumilikia klabu ya mpira na kuisaidia China kukua kimpira kama ndoto za Rais wa nchi hiyo zilivyo. Rais wa China ni rafiki karibu wa Tony Xia na kunauwezekano msimu ujao akazuru Villa Park.Xia aliangalia baadhi ya klabu ikiwemo Everton, lakini alipohudhuria mchezo wa mwisho wa Aston Villa alivutiwa na mwamko wa mashabiki wa timu hiyo akaamua kuinunua.
Maoni
Chapisha Maoni