Msichana wa pili wa chibok aokolewa chini ya boko haram
Jeshi la Nigeria limesema kuwa
msichana mwingine aliyetekwa na wanamgambo wa Boko Haram zaidi ya miaka
miwili iliyopita kutoka shule ya Chibok ameokolewa.
Siku ya Alhamisi msichana mwingine mwenye miaka 19 ambaye alifnikiwa kutoroka katika kambi ya Boko Haram, Amina Ali Nkeki,alipelekwa katika mji mkuu Abuja akiwa na mtoto wake alizaliwa wakati ametekwa, kwa ajili ya kukutana na Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari.
Zaidi ya wasichana wengine mia mbili bado hawajapatikana,huku ikidhaniwa kuwa bado wanashikiliwa katika misitu ya Sambisa karibia na mpaka wa Cameroon.Gavana wa jimbo la Borno amesema kwamba jeshi la nchi hiyo limejiandaa kuwakomboa wasichana hao.

Maoni
Chapisha Maoni