Mtanzania kucheza Europa mwakani
Mbwana
Samatta ameingoza KRC Genk kucheza play off za Europa League baada ya
kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5-1 katika mechi ya pili ya play
off za Ubelgiji.
Ushindi huo umepatikana ukianza na Samatta kusababisha penalti iliyokwamishwa kimiani na Nikos Karelis katika dakika ya 20.
Dakika
7 baadaye Samatta akatupia kabla ya wapinzani wao kupata bao kupitia
Jeremy Perbet na Sandy Walsh akaongeza la tatu kwa Genk.
Kipindi
cha pili, Genk walipata mabao mengine mawili kupitia kwa Karelis huku
wakiwa pungufu mara mbili baada ya wachezaji wao wawili kutolewa kwa
kadi nyekundu.

Maoni
Chapisha Maoni