Mugabe asema kuwa haondoki madarakani
![]() |
| Mugabe akihutubia |
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
amesema kuwa yeye sio Mmarekani wala Muingereza wakati akiwahutubia
karibu watu 50,000, wafuasi wake kwenye mkutano uliofanyika kwenye mji
mkuu Harare kwa heshima yake.
Amesema kuwa yeye anawahudumia watu wa Zimbabwe na kuwa ataondoka tu ikiwa watu wangetaka afanye hivyo. Hata hivyo amesema kuwa haondoki na haendi popote.

Maoni
Chapisha Maoni