Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ne-Yo kushusha bonge la shoo Tanzania


Moto wa burudani utawaka katika jiji la Mwanza Jumamosi ya wiki ijayo ambapo msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva kutoka Marekani NE-YO atakapo shusha bonge ya shoo kwa kushirikiana na wasanii wa hapa nchini katika uwanja wa CCM Kirumba kwenye onyesho lililotayarishwa na Jembe Media chini ya Udhamini wa Vodacom Tanzania.
001.JEMBE
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(Katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,(hawapo pichani) wakati wa kutangaza baadhi ya wanamuziki nchini ambao watatoa burudani pamoja na Mwanamuziki nguli kutoka Marekani NE-YO, katika Uwanja wa (CCM) Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka na Vodacom Festival 2016.Wengine katika picha kushoto ni Mwakilishi wa NE-YO,E.Jay Mathews na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt.Sebastian Ndege

Akiongea juu ya onyesho hilo la kihistoria katika ukanda wa ziwa Magharibi,Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inayo furaha kudhamini tamasha hili kubwa litakaloleta burudani ya muziki kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Aliwataja baadhi ya wanamuziki watakaowasha moto kumsindikiza NE-YO kuwa ni Diamond,Ney wa Mitego,Fid Q,Ruby,Baraka the Prince,Juma Nature,Mr.Blue,Stamina,JJ Bendi na wengineo.
002.JEMBE
Mwakilishi wa Mwanamuzi nguli toka nchini Marekani NE-YO,E.Jay Mathews (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangazwa kwa wasanii watakaotoa burudani pamoja na mwanamuziki huyo katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016, litakalofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wapili (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt. Sebastian Ndege, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, George Sozigwa Mkuu wa masuala ya ulinzi na Usalama wa tamasha hilo
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Dkt.Sebastian Ndege aliwataka wapenzi wa muziki kujitokeza kupata budurani ya mwaka katika tamasha hilo na mipango ya tamasha hilo kubwa imekamilika na kuwataka wapenzi wa muziki wa Mkoa wa Mwanza wakae mkao wa kula wa ya karne.
003.JEMBE
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na jinsi atakavyoshiriki kutoa burudani na kuimba wimbo wa pamoja na mwanamuzi NE-YO wa nchini Marekani katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016,litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt.Sebastian Ndege,Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania
Kuhusiana na viingilio alisema kuwa tiketi zitauzwa kwa shilingi elfu kumi na kuongeza kuwa wanamuziki watakaoshiriki onyesho hili wamejipanga kutoa burudani kisawasawa na kukata kiu ya wapenzi wa muziki wote Nchini.
Alisema tiketi za onyesho hilo zitauzwa katika vituo mbalimbali Nchini yakiwepo maduka ya Vodacom Tanzania,Pia zitapatikana kupitia huduma ya M-Pesa,Katika kuwapunguzia washabiki usumbufu wa kupanga misururu ya kununua tiketi za onyesho hilo pia zitauzwa kwa kupitia huduma ya M-Pesa bila kuwepo na makato yoyote ya kutumia huduma hiyo ambapo watakaonunua tiketi kwa huduma hiyo kutakuwepo na utaratibu maalumu wa kuingia kwenye onyesho cha muhimu ni kutunza namba zao za kumbukumbu ya mhamala wa malipo.Jinsi ya kujipatia tiketi kwa njia ya M-PESA mteja anatakiwa kupiga *150*00# na kuchagua LIPA KWA M-PESA
2. Chagua MANUNUZI
3. Chagua JEMBEKA FESTIVAL
4. Weka namba ya kumbukumbu – 200200
5. Weka kiasi – 10,000
6. Weka Namba yako ya siri na kwa wale wa tiketi za VIP namba ya kumbukumbu ni 200100 bila malipo yeyote yale.
Kwa msaada wa kununua tiketi, piga BURE namba 0800 71 0040

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.