Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ni miaka 3 tangu alipofariki rapper Albert Mangwair (1982-2013)

Ni miaka 3 tangu alipofariki rapper Albert Mangwair (1982-2013)


Leo imetimia miaka mitatu tangu rapper Albert Mangwair alipo afariki dunia nchini Afrika Kusini.
Albert Mangwair maarufu kama Ngwair alifariki tarehe 28 Mei 2013 nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kwa ajili ya shughuli zake za muziki.

Habari kuhusu kifo cha Ngwair zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa kasi sana kitu kilichowashtua watu wengi sana. Zilikuwa kama uvumi tu na wengi waliamini ni utani ambao baadaye ungeisha lakini ikaja kubainika kuwa ni habari ya kweli. Nchini Afrika Kusini Ngwair alikuwa na rafiki yake M TO THE P waliopelekwa kwenye hospitali ya St Helen ya jijini Johannesburg wakiwa mahututi na haikufahamika kwa uhakika kabisa ni nini kiliwapata.

Habari zilivuma kuwa Ngwair amefariki kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha dawa za kulevya. Tuhuma hizi hadi leo hazithibitishwa kama ndicho kitu kilichochukua uhai wa rapper huyo. Marafiki zake wa karibu waliokuwa naye muda mwingi walieleza kuwa kuwa mpaka anapelekwa hospitali alikuwa hajitambui na huenda alifariki akiwa usingizini.

Ngwair alikuwa ni moja kati ya rappers hatari sana kuanzi kwenye freestyle hadi kwenye mziki wake. Kutokana na umaarufu wake aliokuwa nao, taarifa za kifo chake ziliihuzunisha sana Tanzania kwani ni kweli tulipoteza jembe.

Akizungumza na kituo kimoja cha television, TID ambaye alikuwa rafiki wa karibu na Ngwair alisema kuwa anasikitikana sana kumpoteza aliyekuwa rafiki yake kipenzi kwani walikua pamoja na walisaidiana karibia kwenye kila jambo. Aidha TID alitaka yeyote mwenye hati miliki ya nyimbo za marehemu Ngwair, azikazidhi kwa mama yake mzazi ili na mama naye afaidi matunda ya mwanae.

Aidha wasanii nao walieleza hisia zao juu ya kifo cha Ngwair. Profesa Jay alikaririwa akisema “inaniuma sana lakini sina cha kufanya kwa kuwa ni kazi ya Mungu na kazi yake haina makosa, kinachotakiwa ni kumuombea apumzike kwa amani huko aendako.”

“Sidhani kama atanitoka kichwani kwangu, naona kama ametutoroka kwa kuwa hatuhitaji aondoke muda huu lakini hakuna jinsi tutakutana naye siku ya mwisho na nitamweleza machungu yangu na kwa jinsi gani kifo chake kimeniumiza,” alisema Afande Sele.

Albert Keneth Mangwair  alizaliwa tarehe 16 Novemba 1982 Mbeya, Tanzania. Baada ya muda familia yake ilihamia ambapo yamekuwa makazi yao ya kudumu na alifariki tarehe 28 Mei 2013 akiwa na umri wa miaka 31.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.