Headline za sukari zimeendelea katika vyombo mbalimbali vya habari , Leo May 11 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
ameendelea na zoezi la kuchunguza watu wanaodaiwa kuficha bidhaa hiyo
ambapo ametembelea maeneo mawili tofauti na kubaini uwepo wa sukari
inayosadikiwa kufichwa kwenye makontena.
Makonda amekuta makontena yenye sukari 115 ikisadikiwa kuwa ni mali ya Mohamed Interprises
ambapo amaegiza vyombo vya usalama kuchunguza kwanini sukari hiyo haiko
kwenye mzunguko wa biashara, pia kataka kujua ubora wa sukari hiyo
kutokana na taarifa za awali kuonyesha imetengenezwa Brazil huku packaging ikifanyika Dubai.
Katika eneo lingine RC Makonda amekuta sukari zaidi ya tani 1300
ikidaiwa kuwa ni ya viwandani, Mkuu huyo wa mkoa ametoa saa 24 kupatiwa
nyaraka zote pamoja na kuitaka Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA)
kuhakiki ubora wa sukari hiyo.

Maoni
Chapisha Maoni