Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Sanders, Trump washinda jimbo la West Virginia

Sanders, Trump washinda jimbo la West Virginia

Mgombea wa urais wa Democratic Bernie Sanders amempiku Hillary Clinton katika uchaguzi wa mchujo katika jimbo la West Virginia, wakati Donald Trump amenyakua majimbo mawili zaidi
Kwa upande wa Republican, mgombea aliyebaki Donald Trump amenyakua majimbo mawili zaidi.
Bernie Sanders, Seneta wa Vermont mwenye umri wa miaka 74 ameshinda jimbo la West Virginia na kuyaweka hai matumaini yake dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton. Licha ya kushindwa, Clinton bado anapigiwa upatu kuwa mgombea atakayekiwakilisha chama cha Democratic katika uchaguzi wa rais wa Novemba 8.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Salem, katika jimbo la Oregon, ambako Wademocrat watapiga kura wiki ijayo, Sanders alikiri kuwa kampeni yake ingali inakabiliwa na mlima mkubwa "Kwa ushindi wetu usiku huu jimboni West Virginia, sasa tumeshinda chaguzi za awali na mchujo katika majimbo 19, na acha niwe wazi, tupo katika kampeni hii kushinda tikiti ya Democratic".

Amesema watapambana mpaka kura ya mwisho katika majimbo ya Oregon, Kentucky, California, North Dakota na South Dakota. Sanders alishinda wiki iliyopita katika jimbo la Indiana, wakati Clinton akipata ushindi mdogo Jumamosi katika kisiwa cha Pasifiki cha Guam ambacho ni himaya ya Marekani.
Donald Trump Geste Siegesgeste Sanders anasema sasa kibarua kilichopo ni kwa Wademocrat kumwangusha Trump
Ili kupata tikiti ya Democratic, Clinton ana wajumbe 1,700, ikiwa ni 300 zaidi ya Sanders. Ili kuteuliwa, mgombea atahitaji wingi wa kura, au wajumbe 2,383.

 Clinton anatarajiwa kushinda idadi kubwa ya wajumbe maalum 719 – ambao wengi huwa ni maafisa waliochaguliwa na watu wa ndani ya chama – ambayo itamhakikishia ushindi katika mkutano mkuu wa chama mwezi Julai mjini Philadelphia.

Sanders anatumai kujiimarisha kwa kupata ushindi katika majimbo yajayo yakiwemo Kentucky na Oregon mnamo Mei 17. Wagombea wote pia wataangazia uchaguzi wa Juni 7 ambapo wajumbe maakum 700 watashindaniwa, wakiwemo 475 jimboni California ambako Sanders ameelekeza juhudi zake. Na sasa seneta huyo anasema kazi sasa ni kwa chama kujipanga namna ya kumwangusha.

Trump "wito wetu kwa wajumbe wa Democratic ambao watakusanyika Philadelphia ni kuwa wakati tuna tofauti nyingi na Hillary Clinton, kuna jambo moja tunalokubaliana, nalo ni: lazima tumshinde Donald Trump".

Katika upande wa Republican, mfanyabiashara bilionea wa Manhattan Donald Trump mwenye umri wa miaka 64 ndiye mgombea pekee anayetarajiwa kupewa tikiti baada ya wapinzani wake wawili kujiondoa kinyang'anyironi wiki moja iliyopita.

Ushindi wa Trump katika majimbo ya Nebraska na West Virginia umemsogeza karibu kabisa na nafasi ya kupata kura za wajumbe 1,237 anaohitaji ili kutangazwa kuwa mgombea wa Republican katika mkutano mkuu wa chama hicho mwezi Julai

Sasa anaangazia macho yake kwenye uchaguzi mkuu, na tayari ameanza kumtafuta mgombea mwenza. Anasema ameunda orodha ya watu watano au sita ambao wana ujuzi wa kisheria mjini Washington. Trump anatarajiwa kukutana na Spika wa Bunge la Marekani Paul Ryan mjini Washington kesho Alhamisi baada ya Ryan kusema wiki iliyopita kuwa hayuko tayari kumuunga mkono Trump.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.