Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Saudi Arabia yachukizwa na Tangazo la Iran

Iran inashutumu maafisa wa Saudia kwa vifo vya mamia ya mahujaji wake
Saudi Arabia imejibu tangazo la Iran kwamba raia wake hawataruhusiwa kwenda kuhiji Makka mwaka huu,kwa madai ya kwamba mamlaka ya Saudia imetengeneza vikwazo kwa mahujaji wa Iran kushiriki Hijja hiyo.
Hata hivyo Waziri wa Mambo ya nje wa Saudia Adel al-Jubeir amesema kuwa waumini hao wa Kiislam kutoka nchini Iran,wanahitaji kupewa idhini pia ya kufanya maandamano wakiwa nchiniSaudia jambo ambalo halikubaliki.
Iran inalaumu maafisa wa Saudia kwa vifo vya mamia ya mahujaji wake vilivyotokea mwakajana walipokwenda kuhiji.

Professor Mohammad Marandi kutoka chuo kikuu cha Tehran,anasema wa hoja ya Iran, ni kutaka kujiridhisha kama Mahujaji wake watakuwa salama katika Hijja ya mwaka huu
"Raia wa Iran hawana namna. Maoni ya Wairan ni ya hasira na jazba dhidi ya familia ya Kisaudia.

Saudia imewakatalia Wairan matumizi ya Kamera,ambazo ndizo zilizotumika kuonyesha picha za maelfu ya watu waliokufa katika Hijja ya mwaka jana wakiwemo raia wa Iran. Na kwa kuwa Saudia haikulezea mazingira halisi ya vifo hivyo na baadaye ikaomba msamaha,Wairan wanaona bado mazingira hayajawa salama kwao kwa ajili ya Hijja ya mwaka''.
Professor Marandi amesema vurugu zilizosababisha vifo katika Hijja mwaka jana hazikudhibitiwa vyema na serikali ya Saudia
"Saudia ilionyesha bayana kutoheshimu mahujaji,familia zao na kwa miili ya waliokufa, jambo ambalo kwa Wairan halikubaliki. Hivyo Wairan wanataka kujua ni maboresho gani yatafanyika mwaka huu ili waweze kuwa salama zaidi,lakini Saudia hawataki kuweka wazi kwamba ni mabadiliko gani yaliyofanyika,na wakati huo huo viongozi wa dini nchini Saudia wanaamini kuwa Wairan si waumini kamili wa dini ya kiislamu''.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.