Tanzania yajiondoa kuwa mwenyeji CECAFA
Shirikisho a Soka Tanzana (TFF),
limetangaza kuwa halitakuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la timu za
nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama
ilivyopendekezwa.
Awali mkutano mkuu wa CECAFA uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya hiyo ya Kagame.
Lakini badaye ilionekana kwamba Zanzibar hawangeweza kuwa wenyeji.
Kutokana na ratiba ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kipindi cha Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa kwenye michuano ya CAF hatua ya makundi.
Hivyo itakuwa vigumu kwao kushiriki CECAFA, michuano ambayo imepangwa kufanyika Juni na Julai, mwaka huu.


Maoni
Chapisha Maoni