Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tanzania yatoka sare na Korea Kusini

Tanzania yatoka sare na Korea Kusini

                                                               Serengeti Boys
   Timu ya soka ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' leo Mei 19, 2016 imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini katika mfululizo wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).

        Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India, mabao ya Serengeti yalifungwa na Assad Juma katika dakika ya 12 na Maulid Lembe katika dakika ya 87 ambaye alisawazisha baada ya Korea kutangulia kwa mabao 2-1.

     Matokeo hayo yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi tano na kwamba inasubiri matokeo ya mwisho kati ya Korea Kusini na Marekani yatakayotoa mwanga wa timu itakayocheza fainali.

     Serengeti Boys watashuka dimbani tena dhidi ya Malaysia Mei 21, 2016,Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25, 2016 na kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India.

   India imeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya fainali za kombe la dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.