Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tiwa Savage asainishwa na Roc Nation

Tiwa Savage asainishwa na Roc Nation

Jay Z ameripotiwa kukubali kusainishwa kwa msanii wa Nigeria, Tiwa Savage kwenye label yake, Roc Nation.
Tiwa_Savage's_studio_portrait

Kwa mujibu wa ripoti ya Urban View ya Nigeria, Jay Z ameshawishiwa na uwezo wa Tiwa na alikubali kusainiwa kwake May 24. Imedaiwa kuwa deal lilisimamiwa na wawakilishiwa Roc Nation, Briant Biggs na Shawn Pecas.

Hafla rasmi ya kumtangaza kama mwana familia mpya wa Roc Nation haijafanyika na bado label hiyo haijathibitisha. Kama ni kweli, Tiwa atakuwa msanii wa kwanza kutoka Nigeria kusainishwa kwenye label hiyo na kujiunga na Rihanna, Big Sean, DJ Khaled na wengine.

Balozi huyo wa Forte Oil, MTN na Pepsi kwa sasa yupo chini ya label ya Don Jazzy, Mavin Records.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

VIDEO:mtazame RAPPER huyu asieishiwa vituko mtaani

VIDEO:mtazame RAPPER huyu asieishiwa vituko mtaani Rapa kutoka nchini Marekani, The Game ameonekana kwenye kipande cha video kilichozua maswali kwa mashabiki. Kipande hiko cha video kinamuonyesha rapa huyo [The Game] akiwa amekaliwa juu ya kifua chake na msichana anayejulikana kama Maliah Michel ambaye ni mcheza dance wa uchi kwenye klabu ya usiku, Ace of Diamonds iliyopo Los Angeles .Hata hivyo gumegume hilo liliwahi kuhusishwa kuwa na mahusiano na rapa mwingine, Drake.