Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Uingereza kuwapa wafungwa iPads waweze kuwasiliana na familia zao

Uingereza kuwapa wafungwa iPads waweze kuwasiliana na familia zao

Mapitio mapya ya sheria nchini Uingereza yamependekeza wafungwa kupewa teknoligia bora kwa ajili ya wao kujifunza vyema. Na jambo hili litatangazwa pamoja na mabadiliko makubwa yatakayo tangazwa kwenye Hotuba ya Malikia. Wafungwa wataruhusiwa kutoka nje ya Gereza huku wakiwa na tags maalum ili waweze kuanza kufanya kazi ifikapo wiki za mwisho za kifungo chao. David Cameroon amesema hili litakua ni jambo kubwa sana kutokea magerezani tangu enzi za uongozi wa Malkia Victoria.

Imependekezwa kwamba, wafungwa wapewe iPads ili iweze kuwasaidia kuongea moja kwa moja na familia zao. Pendekezo hili linalotarajiwa kukamilishwa na  Michael Gove, ambae ni Katibu wa Sheria nchini humu na vile vile ni mbunge kutoka Surrey Heath
Uchunguzi uliofanywa na The Guardian katika elimu ya gerezani, ndio ulitoa mapendekezo haya ya matumizi makubwa ya teknolojia kwa wafungwa ili waweze kujiendeleza wenye.

Vile vile mapendekezo mengine yanayotarajiwa kuafikiwa ni ya wafungwa kufungwa tags ambazo zitatumika kama vitambulisho na  zitakuwa zikifuatiliwa na satelaiti. Kwa hili pendekezo inamaanisha kwamba wafungwa (wahalifu) watapunguza muda wa kuwa gerezani. Na kwa wale wasio na makosa makubwa na ni wafanyakazi, itawapasa kutumikia kifungo chao wakati wa mwisho wa wiki. Na muda mwingi wote wanatakiwa kuwa maeneo yao ya kazi. Yote hiyo itawezekana kwa wao kuvalishwa hizo tags (vitambulisho) zitakazokua zinafatiliwa na sateliti.

Maelfu ya wafungwa wengine ambao watakua wanakaribia mwisho wa kutumikia kifungo chao, wataruhusiwa muda wa mchana kuenda sehemu watakazo pangiwa kufanya kazi ili waanze kufanya kazi mapema.
Mahakama itatakiwa kutumia sana adhabu yake ya kufanya kazi za kijamii kama njia mbadala ya kuwapeleka watuhumiwa jela.

David Cameroon alisikika akisema, kwa muda mwingi tumeacha magereza yetu yawe imara, sio tu kwamba inaongeza mzungo wa uhalifu, bali pia inaongeza bili kwa walipa kodi ambazo zinaenda kwa watu walishindikana katika jamii, na hakuna sehemu nyingi ambapo wangeweza kubadilishwa zaidi ya humo humo kwenye magereza yetu.  Hivyo basi Jela haitakua tena sehemu ya wafungwa kupumzika, bali itakua sehemu ambayo maisha ya watu wengi yatabadilika’.

Katibu wa Sheria Michael Gove naye alisema, ‘Gereza ni lazima litoe mafunzo zaidi kwa wahalifu, tutawaweka magavana kwenye madaraka, waweze kuwa huru kuamua jinsi ya kuendesha magereza haya jinsi wao wanavyodhani ni sahihi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.