Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ujerumani yachapwa 3-1 na Slovakia

Ujerumani yachapwa 3-1 na Slovakia

Kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya Slovakia katika mchuano wa kirafiki kimempa kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew kazi ya kufanya kabla ya kukichagua kikosi chake cha mwisho cha dimba la Euro 2016

Loew ana mkutano muhimu na madaktari wa timu ya taifa akihitaji hakikisho kuwa wachezaji muhimu wakiwemo nahodha Bastian Schweinsteiger na beki Mats Hummels watakuwa katika hali nzuri kabla ya kuanza dimba la kombe la mataifa ya Ulaya Juni 10 nchini Ufaransa.

Ana hadi usiku wa manane leo kukitaja kikosi chake cha wachezaji 23, baada ya kurejea katika kambi ya mazoezi ya timu ya Ujerumani nchini Uswisi, akiwa na mambo kadhaa ya kutafakari kutokana na kichapo cha 3-1 dhidi ya Slovakia mjini Augsburg hapo jana.

Joachim Löw Kocha Loew anasema ameridhishwa na chipukizi kikosini

Loew aliwapa wachezaji kadhaa chipukizi nafasi ya kumwonyesha uwezo wao "Leo ilikuwa siku ya wachezaji wetu chipukizi, Leroy Sane, Bernd Leno ambao wamecheza kwa mara ya kwanza halafu katika kipindi cha pili, Julian Weigl, Julian Brandt, Joerg Kimmich. Kwa hiyo kulikuwa na shinikizo kubwa katika hali hiyo. Bila shaka huwa kunatokea kosa moja au jingine. Lakini wote wanne wameniacha na hisia nzuri mazoezini".

Loew sasa ana mchuano wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Hungary mjini Gelsenkirchen Jumamosi ili kuipiga msasa timu yake kabla ya Ujerumani kuelekea Ufaransa katika kambi yao ya Evian-les-Bains.

 Alipoulizwa nani atacheza mchuano dhidi ya Hungary, Loew alisema "tutatangaza hilo mara baaa ya kufikia maamuzi. Tutazungumza baada ya kila kitu kutulia, tuangalie mazoezi Jumatatu na tena Jumanne, na kisha tutaamua wachezaji watakaocheza. Tutangaza kwa wakati mzuri wakati tutafikia maamuzi".

Ujerumani – inayotafuta kombe la nne la Ulaya – itaanza kampeni yake ya Euro dhidi ya wapinzani katika Kundi C Ukraine mjini Lille Juni 12, kisha dhidi ya Poland mjini Saint-Denis Juni 16 na Ireland Kaskazini mjini Paris Juni 21.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.