VIDEO: Alichokiongea Mbunge Joshua Nassari baada ya Bunge kukataa kujadili wanafunzi kufukuzwa chuo

May 30 2016 Baadhi ya Wabunge kutoka
vyama tofauti wamegoma kuendelea kushiriki vikao vya Bunge baada ya
kutaka hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
waliotakiwa kuondoka chuoni hapo ndani ya masaa 24.
Naibu Spika Tulia Ackson aliliazimika
kutoa amri ya kutolewa nje kwa Wabunge hao walioonekana kutokubaliana
na kauli ya Bunge kuwa haitaweza kuruhusu mjadala huo ufanyike ndani ya
Bunge.
Alichokiongea Mbunge Joshua Nassari nje ya bunge hiki hapa chini kwenye hii video…
Maoni
Chapisha Maoni