VIDEO: Uchambuzi wa Edo Kumwembe kuhusu Van Gaal kufukuzwa Man United
Bado wapenzi na mashabiki wa Man United wanasubiri ile siku atakayotangazwa rasmi kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Louis van Gaal ndani ya klabu ya Man United, mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe anatoa tathmini yake.
“Ni
kweli Van Gaal alikuwa anahitaji muda zaidi wa kujenga timu, kwani Van
Gaal ana CV kubwa katika vilabu alivyopita ila anahitaji misimu mitatu
minne ili aweze kupata mafanikio, halafu Van Gaal sio kocha wa
kufundisha mastaa huwa anawapa nafasi wachezaji wachanga”
“Kwa
Man United kwa sasa wanahitaji kujenga image ya klabu yao ambayo
itaiwezesha kulinda brand yao ya biashara, hivyo Mourinho ni mtu sahihi
kuitoa shimoni klabu hiyo, kwani Mourinho ni kocha mwenye rekodi ya
kutwaa mataji katika msimu wake wa kwanza”
Maoni
Chapisha Maoni