Vurugu ndani ya Bunge za sababisha Zitto, Mdee, Lissu kusimamishwa kuingia Bungeni
Kufuatia mvutano mkali uliotokea lengo bungeni, adhabu kali zimetolewa kwa wabunge wa upinzani ikidaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya bunge hilo. Baadhi ya wabunge walioonywa na kupewa adhabu ni pamoja na
Wabunge wote wa Upinzani wamepewa onyo kali kwa kung’ang’ania Bunge lionyeshwe moja kwa moja na na kituo cha televisheni ya Taifa (TBC).
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu na na Mbunge wa Bunda Esther Bulaya wamesimamishwa kwa mikutano 2 ya Bunge. Hivyo wabunge hawa hawataingia bungeni hadi mwakani 2017.
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na Mbunge wa Kawe Halima Mdee wamesimamishwa shughuli za Bunge mpaka mwezi Septemba 2016.
Wabunge wengine waliofungiwa ni pamoja na Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul, Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, wamefungiwa kushiriki vikao vilivyobaki vya bajeti. Kwa upande wa Mbunge wa Tarime John Heche, yeye amefungiwa kuhudhuria vikao kumi mfululizo vya bajeti kuanzia leo.
Huu ni uamuzi wa kamati Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge chini Mh George Mkuchika (Mb)
Aidha wabunge wa Upinzani wametoa Hoja ya kutokuwa na Imani na Naibu Spika kwa mujibu wa kanuni ya 138(1) ya Bunge na Ibara ya 85(4)(c) ya Katiba.
Kwa upande wa wabunge wa CCM, akizungumza mbunge Joseph Msukuma ambaye ni mbunge wa jimbo la Geita Vijijini amesema kuwa kusimamishwa kwa wabunge wa upinzani ni fundisho kwa wabunge wengine.
Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga (CCM) yeye amesema kuwa kusimamishwa kwa wabunge ni kwamba ni kujenga heshima kwa Bunge. Aidha ametaka hili liwe fundisho kwa wabunge waliobaki na anaunga mkono hoja kusimamishwa kwao
Maoni
Chapisha Maoni