Wana kijiji 5 wafariki wakitafuta maji India
![]() |
| Ukame nchini India wasababisha uhaba wa maji |
Wana kijiji watano katika eneo
lililokumbwa na ukame kaskazini mwa India wamefariki wakijaribu kutafuta
maji katika kisima kisichotumika.
Eneo kubwa la India linakabiliwa na ukame mbaya ambao umewaua takriban watu 300.
Haryana na majimbo mengine wiki iliopita yalikosolewa na mahakama ya juu nchini India kwa kushindwa kutambua tatizo hilo la maji.
Uhaba wa maji India
Lakini naibu afisa wa polisi katika wilya hiyo Virender Singh alikana kwamba walihitaji maji ya kunywa akisema wanaume hao walitaka kukitumia kisima hicho kwa maji ya kuoga na kuosha.
''Kisima hicho kilikuwa hakijatumika kwa takriban miaka mitano hadi sita na gesi yenye sumu ilikuwa imetanda huko chini'',aliambia kituo cha habari cha AFP.

Maoni
Chapisha Maoni