Mahakama nchini Misri imependekeza adhabu ya kifo kwa watu 25 waliohusika katika mapigano ya kikabila kusini mwa nchi hiyo.
Zaidi ya watu 20 waliuawa katika ghasia zilizotokea miaka miwili iliyopita katika mkoa wa Aswan.
Polisi wanazielezea ghasia hizo kuwa ni mauaji mabaya ambayo hayaja wahi kutokea katika siku za hivi karibuni.

Maoni
Chapisha Maoni