Wazazi wamtelekeza mtoto makusudi Japan
Wazazi wanasema walimtelekeza mwanao kama njia ya kumuadhibu
Wazazi wa mtoto mvulana wa umri wa
miaka saba ambaye hajulikani aliko katika milima iliyo kaskazini mwa
Japan wamekiri kuwa walimtelekeza mvulana huyo kama njia ya kumuadhibu.
Awali wazazi wake waliwaambia polisi kuwa mvulana huyo alitoweka wakati walikuwa wakitafuta mboga msituni.
Lakini baadaye walikiri kumtelekeza mwanao na kusema kuwa waliporudi kumtafuta dakika tano baadaye walipata ametoweka.

Maoni
Chapisha Maoni