YANGA KUTUA KESHO ALASIRI
Mabingwa wa Tanzania, Yanga wanatarajia kutua nchini kesho saa 9:30 wakirejea kutokea Angola.
Inaonekana
mashabiki watajitokeza kwa wingi sana kwa kuwa imekuwa ni gumzo kubwa
kwenye mitandao ya kijamii na wengi wakitaka kujua kikosi hicho
kitawasili saa ngapi.
Yanga
inatua nchini kwa kutumia ndege ya South African Airways wakipitia
Johannesburg, Afrika Kusini ikiwa ni saa chache baada ya kuitoa
Esperanca na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Yanga
sasa itacheza hatua ya makundi ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu ya
Tanzania kushiriki michuano hiyo katika hatua ya makundi.

Maoni
Chapisha Maoni