BINGWA WA KIHISTORIA VPL
Yanga imekabidhiwa taji lao la ubingwa wa VPL msimu wa 2015-16 baada ya kufanikiwa kulitetea taji hilo ambalo walilitwaa msimu uliopita. Yanga imepewa kombe hilo ikiwa na pointi 74 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kutoka sare na Ndanda FC kwenye uwanja wa taifa.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo huo alilikabidhi kombe hilo kwa nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Ndanda FC dhidi ya Yanga.
Ubingwa huo unawafanya Azam FC kulikosa taji hilo ndani ya misimu miwili mfululizo wakati Simba wao wameendelea kulikosa taji hilo ndani ya misimu minne mfululizo.
Mambo muhimu kufahamu
- Yanga wametwaa ubingwa wao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa mara ya 26 kwenye historia ya klabu hiyo
- Ubingwa wa msimu huu ni wa pili mfululizo baada ya kuunyakua msimu uliopita na kufanikiwa kuutetea kwa mara nyingine.
- Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amenyanyua kombe hilo kwa mara ya pili akiwa kama nahodha wa kikosi cha Yanga. Msimu uliopita, Cannavaro alinyanyua ndoo hiyo kwa mara ya kwanza akiwa nahodha wa Yanga aliyerithi majukumu hayo kutoka kwa Shadrack Nsajigwa.
- Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Vicent Bosou, Isoufou Boubabakar, Paul Nonga, Geofrey Mwashiuya, Deus Kaseke, Haji Mwinyi, Benedict Tinoco na Matheo Anthony ni wachezaji ambao wametwaa taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya kujiunga na Yanga msimu huu.
- Yanga walitangaza ubingwa wakiwa na pointi 68 baada ya Simba kupoteza mchezo wao dhidi ya Mwadui, leo walikuwa wanakabidhiwa kombe hilo bila kujali kama wangefungwa, kutoka sare au kushinda dhidi ya Ndanda FC.

Maoni
Chapisha Maoni