Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ZAWADI ZA WASHINDI VPL


Ligi Kuu ya kandanda Tanzania Bara (VPL) itafikia mwisho wikendi ijayo kwa timu zote 16 kucheza game zao za 30.

Tayari bingwa wa msimu huu amekwisha fahamika (Yanga) ambao watakabidhiwa kombe lao siku ya Leo. Hapa nakuletea thamani ya zawadi mbalimbali ambazo wadhamini wakuu wa ligi hiyo kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom watazitoa kwa washindi.

BINGWA KULAMBA TSH. 81 MIL
Yanga itaingiza zaidi ya milioni 81 katika akaunti yao kutokana na kutwaa kwao taji hilo.

MSHINDI WA PILI
Mshindi wa pili katika ligi hiyo anataraji kuvuna kiasi cha milioni 40. Nafasi hii hadi sasa inawaniwa na timu za Azam FC na Simba.

MSHINDI WA TATU
Timu itakayomaliza nafasi ya tatu yenyewe itafanikiwa kujipatia kiasi cha milion 29.

MSHINDI WA NNE
Mtibwa Sugar ikiwa itamaliza katika nafasi ya nne waliyopo kabla ya game mbili za mwisho inaweza kupata milioni 23 kama zawadi ya mshindi wa nafasi hiyo.

MFUNGAJI BORA
Mrundi, Amis Tambwe anasaka tuzo yake ya pili ya ufungaji bora katika VPL. Akiwa amekwishafunga jumla ya magoli 21 hadi sasa, mfungaji huyo bora wa msimu wa 2013/14 anaweza kujiingizia kiasi cha milioni 5.4 kama zawadi ya mfungaji bora.

MCHEZAJI BORA WA LIGI
Mshindi wa tuzo hii msimu uliopita ni kiungo mshambulizi wa Yanga, Saimon Msuva. Unajua mchezaji bora wa msimu atavuna kiasi gani? Ni kiasi cha milioni 5.4.

GOLIKIPA BORA
Kama ilivyo kwa mfungaji bora na mchezaji bora wa msimu, tuzo ya kipa bora pia itaambatana na zawadi ya milioni 5.4.

TIMU YENYE NIDHAMU
Klabu yenye kadi chache na iliyoonyesha uungwana kwa msimu mzima itazawadiwa kiasi cha milion 17.

KOCHA BORA
Tuzo hii ilizua maneno mengi msimu uliopita baada ya Mbwana Makatta aliyekuwa ameisimamia Kagera Sugar kutangazwa mshindi licha ya kwamba alikuwa katika msimu kwa game nane tu. Tuzo ya kocha bora itaendana na zawadi ya milioni 8.

MWAMUZI BORA
Mwamuzi atakayekuwa amefanya vizuri kwa msimu mzima atazawadiwa tuzo na kiasi cha milioni 8 pesa taslim.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.