Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BAADA KUMKOSA VARDY WENGER BADO YUPO LEICESTER, AMLENGA KANTE!

BAADA KUMKOSA VARDY WENGER BADO YUPO LEICESTER, AMLENGA KANTE!


BAADA ya kumkosa Jamie Vardy ambae amethibitishwa kubakia na Mabingwa wa England Leicester City, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hajabanduka kwa Mabingwa hao na sasa ameelekeza nguvu zake kwa Kiungo N'Golo Kante.
Jana Leicester ilitoa tamko rasmi kwamba Straika huyo ambae sasa yuko France akiichezea England EURO 2016 atabakia Klabuni kwake.
Mapema Mwezi huu, Arsenal iliivamia Leicester na kutoa Ofa ya Pauni Milioni 20 ambayo ndiyo imo kwenye Mkataba wa Vardy akitakiwa na Klabu nyingine na kila dalili zilikuwepo kwamba atahamia Emirates.
Lakini Vardy mwenyewe akasita kutoa uamuzi wa haraka na Wiki iliyopita Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, akanyoosha Mikono juu na kuungama kuwa Straika huyo aliefunga Bao 24 na kuipa Ubingwa Leicester atabakia Leicester.
Mara baada ya uthibitisho huo kuhusu Vardy, Arsene Wenger sasa amedokeza nia ya Arsenal kumsaini Kiungo N'Golo Kante Mchezaji mwenzake Vardy huko Leicester City.
Hivi sasa Kante yuko na France akiicheza kwenye EURO 2016 ambako anawika kama alivyofanya akiisaidia Leicester kutwaa Ubingwa wa England Msimu uliokwisha juu ambao ulikuwa Msimu wake wa kwanza Klabuni hapo.
Kitu kinachompa Imani Wenger kwamba Kante wanaweza kumpata ni hatua ya Leicester ya kujitayarisha kwa kumnunua mbadala wa Kante, mwenye Miaka 25, ambae ni Kiungo toka Klabu ya France Nice aitwae Nampalys Mendy.
Licha ya tayari kumnasa Kiungo wa Uswisi Granit Xhaka, Wenger ameeleza: “Ni ngumu kuelezea hili kwa sasa. Kante yupo kwenye Listi ya Klabu nyingi. Na ni eneo ambao tuna Wachezaji wengi. Lakini tutaona nini kinatokea katika Wiki mbili au tatu zijazo. Inaonekana Leicester wamenunua Mchezaji kutoka Nice Nampalys Mendy ambae yupo kama Kante na hilo inaelekea wanajitayarisha kumpoteza Kante, hatujui!”
Wenger alimaliza: “Ukiwauliza Watu 100 Mtaani kama wanataka Kante kuichezea France utapata majibu 100 ya ndio. Amefanya kazi njema katika Gemu mbili na sishangai!”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.