Akizungumza leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Damian Lubuva wakati akimkabidhi Rais Magufuli ripoti ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana alisema kuwa mchakato wa katiba mpya utaendelea.
Jaji Lubuva alizitaja sababu mbili za kuahirishwa kwa mkachakato wa kupiga kura ya maoni. Sababu hizo ni;-
- Kutokamilika kwa uandikishwaji wa wananchi kwa ajili ya kupiga kura. Jaji Lubuva alisema kuwa mchakato huo uliokuwa ufanyike Aprili mwaka 2015, uliahirishwa kwa sababu hadi siku ya kupiga kura ya maoni si wananchi wote waliokuwa tayari wameandikishwa. Hivyo kama mchakato huo ungeendelea ni dhahiri kuwa kuna wananchi ambao wangeshindwa kutimiza haki yao hiyo ya msingi.
2. Sababu ya pili ni uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Jaji Lubuva alisema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi isingeweza kufanya vitu vyote viwili kwa wakati mmoja. Hivyo tume hiyo iliwasilisha serikali mapendekezo ya kuahirisha kura hiyo ya maoni hadi hapo uchaguzi utakapomalizika.
Akihitimisha hotuba yake, Jaji Lubuva alisema kuwa zoezi la upigaji wa kura za maoni sio kweli kwamba lilitelekezwa, bali liliahirishwa kwa sababu hizo mbili. Aidha alisema kuwa zoezi hilo lipo kwenye mchakato na mara taratibu zote zitakapokamilika basi wananchi watapata fursa ya kupigia kura katiba mpya inayopendekezwa.


Maoni
Chapisha Maoni