KOCHA wa Italy Antonio Conte anaamini Timu yake isiyopewa matumaini inaweza kuwaumiza Mabingwa Watetezi Spain ambao watacheza nao Jumatatu ijayo kwenye Mechi ya Raundi ya Mtoano ya EURO 2016 huko France.
Mechi hiyo itakuwa ni kama marudiano ya Fainali ya EURO 2012 iliyochezwa huko Kiev, Ukraine na Italy kubamizwa 4-0 na Spain waliotwaa Ubingwa.
Lakini Kocha Conte, ambae mara baada ya EURO 2016 anaondoka Italy na kutua London kuwa Meneja Mpya wa Klabu ya Chelsea, amesema Kikosi chake kiko imara hasa baada ya kuitwanga Timu ngumu ya Belgium 2-0 katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi lao la EURO 2016.
Italy walifuzu na kushika Nafasi ya Kwanza ya Kundi hilo baada ya Mechi 2 tu na kwenye Mechi yao ya mwisho Conte alibadili Wachezaji 8 na kufungwa 1-0 na Republic of Ireland.
Italy hawana rekodi nzuri dhidi ya Spain kwa Miaka ya hivi karibuni kwani pia walibwagwa kwa Penati kwenye Robo Fainali ya EURO 2008 ambayo pia Spain walibeba Kombe.
Na hata kama Italy wataibwaga Spain hiyo Jumatatu njia yao ya kutwaa EURO 2016 ni ngumu mno kwani Robo Fainali huenda wakakumbana na Mabingwa wa Dunia Germany na wakipita Nusu Fainali huenda wakawakwaa Wenyeji France au England.
EURO 2016
Ratiba
**Saa za Bongo
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Jumamosi Juni 25
Switzerland v Poland (1600, Stade Geoffroy Guichard, St Etienne)
Wales v Northern Ireland (1900, Parc des Princes, Paris)
Croatia v Portugal (2200, Stade Bollaert-Delelis, Lens)
Jumapili Juni 26
France v Republic of Ireland (1600, Stade de Lyon)
Germany v Slovakia (1900, Stade Pierre Mauroy, Lille)
Hungary v Belgium (2200, Stadium de Toulouse)
Jumatatu Juni 27
Italy v Spain (1900, Stade de France, Paris)
England v Iceland (2200, Stade de Nice)

Maoni
Chapisha Maoni