Marais wanne wanaosisitiza nidhamu kwa kiwango cha juu zaidi katika utumishi wa umma barani Afrika
Kufanyia kazi chini ya Marais hawa wa Afrika hatuwezi kusema ni moja ya kazi rahisi duniani. Hawana simile kwa wafanyakazi wasiokuwa kwenye msitari na huhakikisha adhabu inatolewa ipasavyo kwa mhusika. Ni waadabishaji moja kwa moja kutoka moyoni na kwao, kitu cha muhimu zaidi kwao ni kuhakikisha walicho kiagiza kimefuatwa ipasavyo na kimefanyika kwa ufanisi.
Rais Paul Kagame hajafanya siri kuwa na kiu ya kuibadilisha Rwanda kuwa yenye mafanikio kwa kipindi alichokipanga na anaendelea vizuri mpaka sasa. Kiuchumi, Rwanda imeweka rekodi nzuri sana ya mapato ya Taifa (GDP) namba ya ukuaji wake na nafasi yake katika uchumi wa Dunia imekua ni ya kuonewa wivu na majirani zake wengi kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Haya yote yamewezekana kutokana na uongozi wa Kagame na maadili ya kazi. Kwa kuongelea maadili ya kazi, Gazeti la New York Times liliwahi kuripoti kwamba, “hukaa mpaka saa nane au saa tisa za usiku kufuatilia mambo yalioko ‘The Economist’ au akisoma maendeleo ya ripoti za vijiji vya red-dirt vilivyoko katika nchi yake, huku akitafuta njia nzuri zaidi za kuweza kuongeza na kupanua Bilioni zinazopatikana katika Serikali yake kila mwaka kutoka kwa Nchi za wafadhili ambao humuweka kama mfano mzuri sana wa jinsi fedha za wafadhili zinavyoweza kufanya kazi nzuri Afrika.
David Himbara, mwandani wa zamani wa Kagame ambaye sasa anaishi uhamishoni nchini Afrika Kusini.
Himbara anasimulia jinsi Kagame ilivyo wahi kumuita mkurugenzi wa fedha na afisa wa jeshi katika ofisi yake mwaka 2009, na kumsema kuhusu ununuzi wa mapazia ya ofisi na baadae akaita walinzi wawili katika ofisi yake na fimbo na kuwaambia walale chini na kisha kuanza kuwachapa kwa hasira na alipochoka akawakabidhi viboko walinzi wake kuendelea kuwachapa.
Alipoulizwa kuhusu upigaji wake, Kagame hakukataa bali alisema “It’s my nature.” I can be very tough, I can make mistakes like that.”
Kama ilivyokua kwa Kagame, Rais Muhammadu Buhari nae yuko katika harakati za kuiweka nchi yake katika njia sahihi na hakika ya maendeleo kiuchumi. Kama Kagame pia yeye aliwahi kuwa mwanajeshi na alikuwa na sifa kubwa sana ya ukali na anapoagizwa alitekeleza kwa ufanisi na kuleta matokeo. Katika kipindi chake cha kwanza kama kiongozi wa Jeshi Nigeria mwaka 1984, Buhari alikuza sana sifa yake kuwa mwenye kunyoosha nidhamu sana.
Ilikuwa ni katika kipindi chake cha kwanza alipoanzisha kile alichokiita ‘vita dhidi ya utovu wa nidhamu’ katika jitihada za kutaka Wanigeria wapitishe misingi ya kiraia kama kupanda mistari kwenye vituo vya mabasi. Alifanisha hili baada ya kupeleka wanajeshi wenye viboko kwenye vituo hivyo vya mabasi.
Vile vile ‘Vita dhidi ya watovu wa nidhamu’ iligusa hadi wafanyakazi walio chini ya Buhari. Kwa kipindi hicho, watumishi wa Serikali waliofika kazini wamechelewa walirushwa kichura chura ikiwa kama adhabu ya uchelewaji wao.
Na sasa kuna fununu kwamba Buhari anataka kufufua ‘Vita dhidi ya Utovu wa nidhamu’ na kuianzisha upya. Waziri wa Habari na utamaduni Alhaji Lai Mohammed alisema kampeni hizo zitapewa jina ‘mabadiliko huanza na mimi’ na itakua hususani kwa ajili ya kuongeza uadilifu maadili ya kazi kwa ujumla Nidhamu katika Nchi.
Na kama itakua kama ilivyokua mwanzoni, kampeni hii mpya ya uongozi wa Buhari itatikisa sana watumishi wa Umma.
John Pombe Magufuli kwa sasa inawezekana akawa anaongoza kwa kukubalika kuliko Rais yeyote Afrika. Tangu ale Kiapo cha kuongoza Ofisi ya Rais mwaka jana Novemba, amekua katika vita ya kuindoa rushwa, Uzembe na Utoro katika nchi yake.
Alifuta sherehe za uhuru na kuongoza usafi wa mitaa badala yake na vile vile akakata bajeti ya chakula cha usiku iliyopangwa kufanyika kwa ajili ya ufunguzi wa Bunge kwa 90%, na vile vile kutaja idadi pungufu ya mawaziri 11 ya Baraza la mawaziri lilokuwepo kabla ya uongozi wake.
Watanzania wamempenda na kufurahia uongozi wa Magufuli kiasi cha kumpa jina la Tinga Tinga, kwa kile ambacho wanasema hana upendeleo wowote aliteka pia mitandao ya kijamii katika Afrika mashariki mfano Twitter kulianzishwa Hashtag ya #WhatWouldMagufuliDo, msemo ulitokana na jinsi alivyokua akipunguza matumizi kwa vitu visivyo na umuhimu.
Kwake yeye fuata taratibu, na ameshatuonyesha ni jinsi gani usipofuata taratibu ni nini kinatokea. Tangu kuapishwa kwake, Magufuli amesha fukuza watu zaidi 150 katika nyazifa mbalimbaliza kazi, ikiwa ni pamoja na kiongozi mkuu wa kuzuia na kupambana na rushwa. Na wala hajaacha wale aliokua nao karibu kwa lolote. Hivi karibuni alimfukuza Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga, ambaye ni Rafiki yake wa karibu kwa kuingia Bungeni amelewa.
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Rais huyu wa Sudan Kusini ameingia katika ukurasa wetu huu kwa hisani ya post zilizowekwa Facebook na Mabior Garang de Mabior, mtoto wa aliyekuwa mwanzilishi wa Nchi ya Sudan Kusini
Dr. John Garang de Mabior. Kijana huyo Garang, ambae ni Waziri wa vyanzo vya maji alipost Facebook jinsi alivyofukuzwa katika mkutano wa baraza la mawaziri na Rais akiwa amevaa Bow tie.
Kiir ameweka mavazi ya kuvaa kwa mawaziri wake, na bow tai si moja wapo. Lazima iwe tai ya kawaida.
Na hao ndio Viongozi wane Afrika, wanaongoza kwa kuzingatia Nidhamu. Inaweza kuwa jinsi ya kutenda na Usimamizi wake ukawa sio wa kawaida, lakini vichwani mwao wakawa wanaona ni sahihi kwa zile changamoto Nchi zao zinakabiliana nazo.
Maoni
Chapisha Maoni