Pam D aeleza sababu ya kubadilisha producer kwenye wimbo mpya aliomshirikisha Nay wa Mitego
Akiongea Pam amesema wimbo wake mpya Nipe Nono aliomshirikisha Nay wa Mitego umetayarishwa na Mr T Touch.
“Nilitaka watu waone kuna utofauti sio kila siku Mesen tu mwisho wa siku watu watakuwa wanasema Pam bana anabebwa na Mesen kwahiyo ilinibidi niamue kufanya katika studio nyingine,” alisema.
Wimbo huo utatoka Ijumaa hii.
Hivi karibuni Mr T Touch ambaye ni producer wa Free Nation amekuwa akitumiwa na wasanii wengi na miongoni mwa watayarishaji wanaokubalika zaidi kwa sasa.
Maoni
Chapisha Maoni