Drake na Eminem wote wameweka picha hii kwenye akaunti zao za Instagram
Usiku wa Jumanne, 16 August, ziara hiyo ilikuwa katika ukumbi wa Joe Louis Arena mjini Detroit. Rapper huyo mwenye asili ya Canada alishindwa kujizuia na kumkaribisha mwenyeji wa mji huo rapper Eminem katika steji na kutumbuiza wimbo walioshirikiana mwaka 2009, Forever.
Wawili wao walidhaniwa kuwa na beef lakini tetesi hizo zilimalizwa mara baada ya Drake na Eminem kumaliza kutumbuiza. Drake aliwaambia mashabiki wake waliohudhuria tamasha hilo kuwa wampigie shangwe Eminem kwa kusema, “Make some noise for the greatest rapper to ever get on a microphone – he goes by the name of Eminem.”

Mkongwe huyo wa rap pia aliongezea na kusema ni heshima kubwa kutumbuiza jukwaa moja na Drake.Vile vile Drake katika tour yake hii amekuwa akipewa support na mastaa mbalimbali duniani wakiwemo Rihanna, Kanye West, LeBron James, French Montana, Cam’ron , Juelz Santana, J. Cole, Fat Joe , Remy Ma na wengine.

Maoni
Chapisha Maoni