Ruka hadi kwenye maudhui makuu

EATV kutoa tuzo kwa wasanii

Katika kuleta chachu ya sanaa hapa nchini kituo cha Televisheni cha East Africa(EATV) kimeanzisha tuzo za wasanii ambazo zitafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mwezi Disemba mwaka huu.
Akiongea wakati wa kutangaza uzinduzi wa tuzo hizo katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa masoko wa kituo cha televisheni cha EATV,Roy Mbowe alisema kuwa tuzo hii ni kwa ajili ya wasanii wa tasnia mbalimbali na kwa kuanzia mwaka huu itawahusu wasanii wa tasnia ya muziki na filamu katika nchi za Afrika Mashariki.
“Pengine mnaweza mkajiuliza kwanini EATV imeamua kubeba jukumu hili la utoaji tuzo za EATV. Kwa wafuatiliaji wa mambo ya kimataifa watabaini kuwa vituo mbalimbali vikubwa duniani kama kilivyo kituo cha EATV vimekuwa vikitoa tuzo na sisi tukaona kwanini tusipende kazi za wasanii wa kwetu kwa kuzizawadia tuzo na kuzikuza,” alisema.
Alisema utoaji wa tuzo hizi unaanza mwaka huu na hafla ya utoaji tuzo itafanyika Disemba 10 na kituo bado kinaandaa mchakato mzima wa jinsi ya kushiriki kuwania tuzo,vipengele vitakavyoshindaniwa ambavyo alidai kuwa vitatangazwa baadaye na aliishukuru kampuni ya Vodacom kwa kutoa udhamini wa tuzo hizi zenye lengo la kutoa motisha kwa wasanii.
Mbowe aliishukuru serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kutoa kibali cha kuendesha zoezi hili ambalo linalenga kukuza sanaa na kuboresha maisha ya wasanii “Tunatoa shukrani kwa serikali ya Tanzania kutuunga mkono na tutaendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali kuboresha tuzo hii,”alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella alisema Vodacom inafurahi kudhamini tukio hili muhimu lenye lengo la kuwapatia motisha wasanii wa kanda ya Afrika Mashariki.
“Moja ya dhamira ya kampuni ya Vodacom ni kuibuka na kukuza vipaji ndio maana kampuni imekuwa mstari wa mbele kudhamini michezo na Sanaa kwa kuwa inaamini kupitia sekta ya michezo watanzania wengi mbali na kupata burudani inawezesha kuongeza wigo wa ajira na kampuni itaendelea kuwezesha wasanii na wanamichezo kama ambavyo hivi sasa inavyodhamini ligi ya soka ya Vodacom Premier League na mashindano ya kucheza muziki wa dansi yanayojulikana kama Dansi 100.
Afisa Uhusiano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Aristides Kwizera alipongeza kituo cha EATV kwa kuanzisha wazo lenye lengo la kukuza tasnia ya sanaa nchini na aliipongeza Vodacom kwa kudhamini tukio hili.
“Serikali kupitia BASATA iko pamoja nanyi kwa kuwa imedhamiria kuinua vipaji vya sanaa na kkuwawezesha wasanii kujiajiri hivyo tutaendelea kuwaunga mkono wakati wote na natoa wito kwa wasanii kujitokeza kuchangamkia fursa hii ambayo imejitokeza kwa ajili ya kuwatangaza na kuwawezesha kujipatia mapato kupitia kazi zao za sanaa,” alisema.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.