Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kilichomkuta Sitti Mtemvu chamkuta Miss World Kenya

Kilichomkuta Sitti Mtemvu chamkuta Miss World Kenya

Baada ya mrembo wa Tanzania Sitti Mtemvu mwaka jana kupokonywa taji lake la Miss Tanzania na kwenda kwa Lilian Kamazima kutokana kashfa ya umri, huko nchini Kenya aliyekuwa Miss World Kenya 2016 , Roshanara Ebrahim, amepokonywa taji lake baada ya kukumbwa na sakata.

Kwa mujibu wa gazeti la The Standard nchini Kenya, Roshanara mwenye umri wa miaka 23, alishinda taji la mwaka uliopita na alikuwa anatarajiwa kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya Miss World, mwishoni mwa mwaka huu.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na wasimamizi wa Miss World Kenya, kampuni ya bidhaa za urembo, Ashleys imeandika,
“Kuanzia sasa, Roshanara hatoiwakilisha Kenya nchini na hata kimataifa kama Miss World. Tumefahamishwa kuhusu sakata kubwa inayomkumba Roshanara Ebrahim, ambayo inakiuka sheria na masharti ya Miss World Kenya. Tunatekeleza sheria zetu na tunatarajia wanamitindo wetu kusimamia maisha yao ya kibinafsi,”
Kulingana na gazeti hilo , Roshanara ameandika kukubaliana na uamuzi huo na kuwasihi warembo wenye umri mdogo kuhakikisha maisha yao ya kibinafsi, hayaathiri jukumu lao la Miss World.
”Nakaribisha uamuzi wa ofisi ya Miss World Kenya kunipokonya taji la Miss World Kenya kwa masikitiko makubwa, namtakia atakayechukua nafasi yangu kila la heri” alisema Mrembo huyo.
Kabla ya uamuzi wa ofisi ya Miss World Kenya, Roshanara alilazimika kujitetea dhidi ya madai yaliomhusisha kuwa na uhusiano na mwanasiasa mashuhuri.
Tayari ofisi ya Miss World Kenya, imeahidi kumtangaza mwanamitindo atakayejaza pengo lililoachwa na Roshanara Ebrahim siku chache zijaazo.
Roshanara anayesomea uwakili, anatarajiwa kuendelea na shughuli zake za kuwasaidia watoto walio na mpasuko wa mdomo, yaani ‘cleft.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.