Professor Jay kutoa album mpya
Msanii mkongwe wa hip hop Tanzania ambaye kwa sasa ni mbunge wa mikumi amewashangaa wasanii kushindwa kutoa album kwa kisingizio kuwa soko la album limekufa.
Akiongea kwenye mahojiano yake na kipindi cha funiko Base cha radio 5 Jay amedai kuwa album ndio kipimo sahihi cha kupima uwezo wa msanii na kuweka wazi kuwa yuko mbioni kuachia album yake ya tano.
“Album ni haki ya mashabiki,no matter what happens,album ni kipimo kizuri cha kumpima msanii kwamba yukoje,huwezi kupima uwezo wa mtu kwenye single.Kama mimi binafsi niko mbioni kwenye kumalizia album yangu,huu wimbo wa kazi kazi upo kwenye project ambayo itakuwa album ya tano kama solo artist” alifunguka Jay na kushauri wasanii watafute njia mbadala ya kuuza album zao badala ya kulikimbia tatizo
.
.
Maoni
Chapisha Maoni