RayMond anavyojisikia baada ya kufanya wimbo wa Chuma na Chid Benz
Mwimbaji RayMond kutoka WCB amefunguka na kusema kuwa hachukulii poa kufanya kazi na msanii mkubwa kama Chid Benz.
RayMond ambaye ameshirikishwa kwa kuimba kiitikio kwenye wimbo mpya wa Chid Benz unaoitwa Chuma ameweka wazi kufurahishwa kwake kufanya kazi na msanii huyo na kudai kuwa ni ishara kwamba muziki wake unaenda kwenye nuru.
“Ukiachilia mbali mtu niliye fanya naye kazi,ngoma ya chuma naipenda tu ilivyo,pia nilifurahi kupata nafasi ya kufanya ngoma na Chid Benz kwa sababu ni msanii mzuri na mkongwe kufanya naye ngoma inaonyesha kwamba muziki wangu unaenda kwenye nuru.nimefurahi sana sana” alifunguka RayMond ambaye anatamba na wimbo wake wa Natafuta KIKI
.
.
Maoni
Chapisha Maoni